Posts

Showing posts from August, 2017
Kibainisho Muhimu Ukumbusho Wa Kuzuia Kukata Kucha Na Nywele Kwa Anayetaka Kuchinja Na Faida Mbali Mbali Kuhusu Hajj Kibainisho Muhimu تَقَبَّلَ اللهُ مِنَّا وَمِنْكُمْ   Allaah Atutakabalie Sisi Na Nyinyi 'Arafah 9 Dhul-Hijjah itakuwa ni Alkhamiys tarehe 31 Agosti 2017M. 'Iydul-Adhwhaa 10 Dhul-Hijjah itakuwa Ijumaa tarehe 1 Septemba 2017M. Ukumbusho Wa Kuzuia Kukata Kucha Na Nywele Kwa Anayetaka Kuchinja Tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa, wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa (anayewakilisha mtu kumchinjia), kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele za mwili na kucha mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:    عن أم سلمة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ)) وفي رو...