MAZAZI YA MTUME MUHAMMAD(S.A.W)

1 MWANGAZA 1 Naanza yangu qauli Kwa jina lake Jalali Alomleta Rasuli Kuiongoa duniya 2 Reh'ema zake A'zizi Zishuke kwa Mwokozi Kipenzi chake Mwenyezi Na Aali zake jamiya 3 Na S'ahaba zake bora Wenye nyoyo za imara Walo kwetu ni ishara Kama nyota samawiya 4 Tukisha Mola h'imidi Na kus'alia H'amadi Tutaje ya Maulidi Ya maisha ya Nabiya 5 Ulimwengu uli kiza Hauoni muwangaza Kila jema wapuuza Maovu wakakamiya 6 Fikira zilichafuka Na nyoyo zilitibuka Ya kweli yalifichika Urongo ukaeneya 7 Ulitoweka muruwa Wabora wajishauwa H'ata Mola azuliwa Kuzaliwa na Mariya 8 Mapadiri na kuhani Walijijenga yaqini Ni nani huyo ni nani Muweza wa kuzuiya 9 Walijipa utukufu Reh'ema kuzis'arifu (Ewe mja mpungufu) Na dhambi kughufiriya 10 Nako huko A'rabuni Kufuru yatia kani Ndiyo nyumba ya Shet'ani Ndiko aliko hamiya 11 Kaa'ba yake Karimu Alojenga Burahimu Ikajazwa masanamu Zaidi thalatha miya 12 Na kiza kilipo kaza Alitengeza Muweza Kuuleta mwangaza Kwa kuzaliwa Nabiya 13 Na mwaka tawambiani Alo zaliwa Amini Mia tano sabii'ni Na moja wa shamsiya 14 Ni mwezi Mfungo Sita Qarini zilizo pita Ulimwengu ulipata Mtume kumpokeya 15 Mwezi huu mtukufu Alizaliwa Sharifu Mjiwe mtakatifu Maka nchi H'ijaziya 16 Kazaliwa Muungwana Na mamiye Bi Amina Na babiye wetu Bwana Alisha mtanguliya 17 Akatunzwa na babuye Na khalafu na a'miye Na walo mlea yeye Baraka na Saa'diya 18 Na huyo Mwana Baraka Ni mama Muafirika Na Saa'diya pulika Ni H'alima A'rabiya MAFUNZO Tunalo jifunza katika mlango huu ni kuwa upotovu ukizidi mno ndio huja uwongofu. Waingereza husema: "The darkest hours are just before dawn". Saa za kiza kabisa ni zile za karibu mno na alfajiri. Ndio Muhammad s.a.w. kazaliwa kwa wakati wake. Nasi tutaraji faraji dhiki zinapo shtadi.  

Comments

Popular posts from this blog