HADITHI 40

   

1. ADDIYNUN-NASIIHATU
Dini ni nasaha
Yaani ni nasaha kwa viumbe au kwa Mtume au kwa
Mwenyezi Mungu. Ndiyo kusema kuwahurumia viumbe, kuishika
dini ya Mwenyezi Mungu kwa uaminifu na kumsaidia Mtume
katika kazi alizokabidhiwa na Mwenyezi Mungu.

2. IJTANIBUL GHADHWABA
Jiepusheni na hasira
Mara nyingi hasira inaleta matusi, magomvi na hata kuuana.

3. ADDUU ZAKAATAKUM
Toeni zaka zenu
Maana zaka ni msaada kwa mafukara na maskini na pia inatakasa
mali ya mtu anayeitoa.

4. IHFADH LISAANAKA
Linda ulimi wako
Yaani usiwe na masingizio, uongo, utesi na maneno ya magomvi,
machafuko, na maneno ya upuuzi.
5. ARHAAMUKUM ARHAAMUKUM
Ndugu zenu ndio ndugn zenu
Kwa hiyo wahurumieni, watendeeni mema, na wasaidieni zaidi
kuliko wengine maana mmechangia damu.

6. ARSHIDUU AKHAAKUM
Waongozeni ndugu zenu
Kwa kuwafundisha na kuwapa mawaidha na kuwakataza maovu
ili wawe watu wema.
Üû ×øŠû iø Üû ×ô ‰û ]ø
7. ASLIM TASLAM
Silimu utasalimika
Mwenye kuishika dini ya Kiislamu huepukana na kila namna ya
upotevu uangamizao. Mwili wake, vitendo vyake na kikao chake
husalimika na mambo yanayomletea maafa na aibu.

8. ATWI’ ABAAKA
Watii wazazi wako
Maana wametufanyia hisani kubwa kwa kutulea na kutusaidia na
kututakia kila jambo la kheri. Basi ni wajibu wetu kulipa hisani
yao kwa kuwastahi na kuwatii na kuwatendea kwa upole na adabu
nyingi.

9. I’TAKIF WA SUM
Kaa katika i’tikafu na funga saumu
Mwislamu anaposhinda msikitini siku tisa au kumi za mwisho za
Ramadhani anapaswa kufunga saumu vile vile. Lau kama ashikwe
na maradhi na kuacha saumu basi atoke msikitini pia, maana
i’tikafu haiwi pasipo saumu.
10. A’LINU NNIKAAHA
Itangazeni ndoa
Kuoana kusiwe kwa siri. Amri hii imejaa hekima, Ndoa
isiyotangazwa hadhara ya watu si halali.
11. AKRIM-I-SHSHA’RA
Ziheshimu nywele
Imewekwa kanuni nzuri ya kuwaheshimu wazee ambao
7
wamekwisha kula chumvi nyingi. Wanastahiki kuheshimiwa na
wadogo wao. Pia maana yake ni kwamba mtu ambapo huwa
amekuza nywele inamlazimu aziangalie vizuri, zisiachwe tu kama
washenzi.

13. ISHFA’UU TU’JARUU
Ombeeni, Mtapata ujira
Tukiona mtu ananyimwa haki yake tusikawie kumwombea kwa
wakuu wake. Naam, uombezi katika dhuluma na ujeuri hauna
kheri kwa yo yote.
12. AL-AIMANU FAL AIMANU
Wa kulia tena wa kulia wake
Inapendeza kufanya kazi zote njema kwa mkono wa kulia. Watu
wakikaribishwa vyakula, wa kulia apewe kwanza tena wa kulia
wake na kadhalika. Na walapo wao wautumie mkono wa kuume.
14. AL-A’MAALU BILKHAWAATIIMI
Matendo hupimwa kwa mwisho wake
Yaani mtu akiendelea na matendo mema mpaka kufa kwake
atahesabika kuwa mwema, na matendo hayo yakikatika yakawa
maovu baadaye akafa hali yu mwovu, basi atatendewa kama mtu
aliyepotea njia. Tunaonywa tusijivunie mema tuliyoyafanya wala
8
tusikate tamaa tukiisha tenda maovu kwa bahati mbaya, maana
twaweza kujisahihisha na kuachilia mbali yamchukizayo Mungu.

15. UUSWIIKUM BIL JAARI
Nawausieni juu ya jirani
Dini ya Kiislamu imetia mkazo juu ya kuwatendea wema majirani.
Jirani na awe mtu namna gani anastahiki kuangaliwa vizuri.
Kuoneana huruma hukuza mapenzi na amani.
16. AKRIMU AULAADAKUM
Waheshimuni watoto wenu
Mtoto wa leo ni baba wa kesho. Lazima tuwafunze kujiheshimu
na hivyo watakuwa na moyo wa kujitoa katika yale yanayowaletea
aibu na pia watashika adabu njema ya kuwaheshimu wengine,
wakubwa kwa wadogo. Kuwatolea ukali kila mara si vizuri.
17. AL-AMAANATU ‘IZZUN
Kuaminiwa ni heshima
Yafaa Mwislamu akae duniani kwa jinsi itakayompelekea
kuaminika. Mtume s.a.w. al ipewa lakabu ya ‘Alamin’
(mwaminifu) na watu wake tangu alipokuwa kijana kwa sababu ya
maisha yake yaliyotukuka. Mhaini hana heshima.
9

18. BAJJILU-L-MASHAAIKHA
Waheshimuni wazee
Kwani wameona ambayo sisi hatukuyaona. Elimu na maarifa
waliyo nayo yatatufaidisha kat ika maisha yetu, na kwa
kuwadharau tutajinyima kheri nyingi.
19. TA’ALLAMUL-YAKIINA
Jifunzeni yakini
Yakini maana yake ni kujua jambo fulani kwa hakika kuwa
ndivyo. Yakini ndiyo msingi wa matendo yote. Mtu mwenye
yakini kuwa mbegu zikipandikizwa zitaota ndiye anayeweza
kuzitoa ghalani na kuzifukia ardhini. Watu ambao imani yao
inalewalewa hawafiki mahali.
20. TAHAADUU TAHAABBUU
Pelekeaneni zawadi mpendane
Kupelekeana hedaya kunazidisha mapenzi. Mtu hali riziki ya
mwigine lakini ni njia bora ya kuunga watu pamoja. Kurani
Tukufu yasema, Mwislamu akiletewa zawadi na arudishe bora
kuliko ile au sawa na aliyopewa.

21. ATTA’ZIYATU MARRATAN
Kupeleka rambirambi kuwe mara moja tu
Ni desturi mbaya kukusanyika mahali pa matanga na kukaa hapo
hapo siku nyingi kuwatia gharama waliofiwa. Mtu aliyepatwa na
10
msiba lazima apewe mkono wa tanzia maana atafarijika lakini
kuiendeleza muda mrefu kutamwongezea huzuni na mzigo.

22. AL-KHAALATU WAALIDATUN
Dada ya mama ni mama
Mtu amheshimu dada ya mama yake kama mama mzazi.
Na pia mtu akifiwa na mkewe akahitaji kuoa tena yafaa mchumba
wake awe dada ya mkewe marehemu maana ataweza kutunza
watoto wake na nyumba yake kama dada yake.
23. ADDU’AAU HUWAL’IBAADATU
Maombi ndiyo ibada
Mwislamu ambaye anamaliza sala yake upesi upesi bila ya
kuomba mahitaji yake kwa Mwenyezi Mungu sala yake haina
maana.

24. ADDUNYA MAZRA’ATUL - AAKHERATI
Dunia ndivo konde la Akhera
Kila mtu ni mlimaji na cho chote atakachotenda katika
maisha ya dunia mfano wake ni kama mbegu ipandwayo kondeni
na yeye atakwenda kuvuna matunda yake baada ya kufa kwake.
Basi na aangalie apandacho.

25. SUUMUU TASWIHHUU
Fungeni saumu mtapata afya
Kama mtu afanyaye kazi siku zote bila kulala au kupumzika
11

huzeeka upesi hivyo tumbo la mtu likishurutishwa kufanya kazi
yake daima halina hudi kuchoka upesi na kudhoofika. Basi kula
shibe siku zote kunadhuru afya na tumbo halipati nafasi ya
kupumzika. Zaidi ya chakula tukitumiacho hakibadiliki kifae
mwilini bali kinapita tu pasipo kufaa cho chote. Kikitumiwa kiasi
kinaleta afya na kujenga mwili. Mojawapo katika faida za saumu
ni kutupatia uzima wa miili yetu.
26. AL’AINU HAQQUN
Kijicho ni haki

27. AS-SABRU RIDHAN
Subira ni ridhaa
Subira siyo kuvumilia taabu na hali mna mnung’uniko moyoni.
Bali hakika ya subira, kama alivyosema Mtume, ni kuridhika na
tendo la Mwenyezi Mungu liwe la kutupendeza au kutuchukiza.

28. AL-MUHTAKIRU MAL’UUNUN
Azuiaye bidhaa anapatwa na mashaka
Islamu inaruhusu biashara ya kawaida lakini inakataza tamaa ya
kupata mali kwa njia isiyo halali. Watu wengi siku hizi hawataki
kuwauzia wenzao bidhaa ili wapate kupandisha bei na kuchuma
mali nyingi. Ijapo bidhaa inajaa ghalani lakini inazuiwa
kuighalisha na kutaabisha wanunuzi. Hiyo inaleta taabu kwa kila
mtu. Watu wasipopata mahitaj i yao kwa bei ya kawaida
huchukiwa sana na matendo ya wachuuzi na udanganyifu, wizi,
12
unyang’anyi na kutoaminiana huonekana katika nchi. Pengine vitu
huchomwa moto. Matukio hayo yaleta dhara kwa wenye biashara
na kwa serikali na wenyeji pia. Watu hao wataadhibiwa na
Mwenyezi Mungu kwa sababu ya choyo na ubahili.

29. AL-MUSLIM AKHUL-MUSLIM
Mwislamu ni ndugu wa Mwislamu
Udugu wa dini huunganisha watu kama uungavyo ujamaa wa
damu. Tunaweza kusema ya kuwa wenye imani kamili wanakuwa
tayari kuachana na jamaa zao kwa ajili ya dini. Basi Waislamu
tusighafilike na wajibu wetu wa kuwatumikia ndugu zetu
Waislamu kwa njia yo yote iwezekanavyo. Udugu huu ukilegea
Waislamu watatengana nayo ndiyo alama ya kupungua imani.

30. AL-MAT’UUNU SHAAHIDUN
Mwenye kufa na tauni ni shahidi
Tauni ni ugonjwa mbaya sana ambao unampa mtu udhia mkubwa
mno. Mwislamu anayeugua ugonjwa huu ameitwa shahidi kwa
sababu hupata taabu nyingi duniani. Na Mungu Mwenye huruma
hataki kumwadhibu mara ya pili katika Akhera.

31. LAA WASIYYATA LI WAARITHIN
Hapana wasia kwa warithi
Sheria ya Islam imeweka sehemu maalumu kwa ajili ya jamaa
fulani ya karibu katika mali yanayoachwa na maiti. Mathalan, mke
katika hali moja anapokea sehemu ya nne (1/4) ya urithi wa
mumewe marehemu na katika hali nyingine apata sehemu ya nane
13
(1/8). Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu na mumewe hana haki ya
kumwongezea kitu cho chote. Naam, anaweza kufanya wasia wa
thuluthi ya mali yake kumpa rafiki zake au jamaa zake wasio na
sehemu maalumu katika urithi au mayatima au kwa ajili ya dini.
Kwa njia hii M wenyezi Mungu amezuia mtu ye yote asipokee
mali nyingi peke yake. Watu wengi wakipata mali kidogo ni bora
zaidi kuliko mtu mmoja kupata mali yote. Ndiyo njia ya amani,
raha, na starehe.

32. LAA TA’UD FII SADAKATIKA
Usirejeshe sadaka yako
Ukiisha kutoa chochote kuwa sadaka haipendezi kutamani
kuichukua tena. Hata Mtume s.a.w. alikataza kukinunua
kilichotolewa sadaka, maana alihofia pengine aliyepewa sadaka
atapunjwa. Mwislamu hawi mchoyo.

33. ANNADAMU TAUBATUN
Majuto ndiyo Toba
Katika maneno haya mawili Mtume ameeleza hakika ya toba ni
nini. Mkosaji apatwapo na majuto juu ya kitendo chake na
anaazimu kwamba hatotenda maovu tena hupokewa kwenye
baraza ya Mungu mwenye huruma. Rehema ya Mwenyezi Mungu
inamfikia kila anayesikitikia matendo yake mabaya na yu tayari
kuyaachilia mbali.

34. IJTANIBUU KULA MUSKIRIN
Jiepusheni na kila kilevyacho
Sheria ya Islam ndiyo ya kwanza kukataza vileo. Pombe za kila
14
aina, bangi, kasumba na namna nyingine yo yote ya kileo, kidogo
au kingi, kimeharimishwa. Hasara ya mali na madhara ya vileo
kwa mwili na akili ya binadamu vimethibitika siku hizi.

35. LAA TATAMANNAWUL-MAUTA
Msiitamani mauti
Watu wengi wanapochukiwa na jambo fulani wanaj iua.
Hilo ni ujinga wa mwisho. Islamu inamfunza mtu asikate tamaa
katika hali zote na afululize bidii na jitihada. Mwislamu
ameumbwa kushinda na kutawala yote yaliyo kinyume chake.
Anayeshindwa na kukata tamaa hawezi kuwa Mwislamu. Mtume
s.a.w. alikataza kumsalia mtu aliyejinyonga, maana hakutegemea
fadhili za Mwenyezi Mungu. Wanywaji wa pombe, kwa kawaida,
huwa wepesi wa hasira na wanataka kujiokoa na maumivu kwa
kujinyonga.

36. ASSALAAMU QABLAL KALAAM
Maamkiano yawe kabla ya mazungumzo
Ni adabu njema kumsalimu mtu kabla ya kusema naye maneno yo
yote.

37. TARKUD-DUA'AAI MA'SIYATU
Kuacha kuomba ni dhambi
Maombi ndiyo sehemu kubwa ya ibada ya mwanadamu.
Hata mtu akifanya kila tendo la heri kama kuwasaidia wenzake na
kuhurumia kiumbe cha Mungu na kutazama wagonjwa na
kutumikia maskini na wenye haja lakini anaacha kumuomba
Mwenyezi Mungu bila shaka amepungua wema, bali ni mwenye


dhambi, maana tumeamuriwa kuomba na asiyedumisha maombi
amevunja amri. Maombi hutuvutia baraka na rehema za Mwenyezi
Mungu na hutuondolea mabalaa mengi yanayotaka kutuangamiza.
38. ZIN WA ARJIH
Pima na uongeze
Kumpa mtu haki yake ni uadilifu, na kumwongezea ndiyo ihsani.
Mtume s.a.w. ataka watu wapendane kwa kutendeana wema wao
kwa wao. Wafanya biashara wamehusika sana na amri hii.
Kumnyang’anya mtu haki yake ni mbali kabisa na mafunzo ya
Islam.
39. ITTAQULLAAHA FIN-NISAAI
Mwogopeni Mwenyezi Mungu juu ya wanawake
Maana wao ndio viumbe dhaifu wasioweza kulinda haki zao
wenyewe. Basi wanaume wanaonywa wasiruke mipaka kwa
kutojali haki zao. Ingawa dunia inaonekana kama imeendelea sana
siku hizi lakini wanawake mpaka sasa wananyimwa haki zao.
40. TALABUL-HALAALI JIHAADUN
Kutafuta riziki ya halali ni jihadi
Uislamu unatufundisha kushika njia ya halali katika mambo yote.
Siku hizi unyang’anyi na udanganyifu vimetapakaa kila mahali na
imekuwa rahisi sana kupata mali kwa njia zilizokatazwa na sheria
ya Mwenyezi Mungu. Basi huwa shida kabisa kupata riziki ya
halali na mtu asipoangalia sana mara huangukia haramu na mali
iliyo najisi. Inatakiwa juhudi kubwa na uangalifu mwingi katika
kupambanua kati ya haramu na halali. Kwa ajili hii Mtume s.a.w.
alisema kwamba mwenye kutafuta riziki ya halali atapata thawabu
kama yule aliyepigana vita katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Comments

Popular posts from this blog