NASAHA YA LEO
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada: Kutawasali Kwa Kutaja Hali Na Kutaja Sababu
Nasiha Mbali Mbali
Inafaa kutawassal kwa kutaja hali au sababu ya jambo unaloliombea du'aa. Ikiwa jambo unaloliomba ni kwa ajili ya manufaa ya dunia, basi liwe ni jambo lenye kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na linalokubalika katika shariy’ah.
Mifano mingi imo katika Qur-aan waliyoomba Manabii. Mifano michache ifuatayo:
Nabiy Nuwh ('Alayhis-Salaam):
Aliomba nusra baada ya kushindwa kuwalingaia watu wake miaka mia tisa na khamsini. [Al-‘Ankabuwt 29: 14].
Katika Suwratul-Qamar Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُونٌ وَازْدُجِرَ ﴿٩﴾
Walikadhibisha kabla yao kaumu ya Nuwh, wakamkadhibisha mja Wetu, wakasema: “Majnuni.” Na akakaripiwa.
Nabiy Nuwh ('Alayhis-Salaam) akaomba:
فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانتَصِرْ ﴿١٠﴾
Basi akamwita Rabb wake kwamba: “Hakika mimi nimeshindwa nguvu basi Nusuru.” [Al-Qamar: 9-10]
Hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamtakabalia du’aa yake Akamuokoa Akawaangamiza madhalimu:
Endelea
Hadiyth Arubaini - Imaam An-Nawawy: 02 - Kuja Kwa Jibriyl Kuwafundisha Waislamu Mambo Ya Dini Yao
Hadiyth Ya Wiki
Hadiyth Ya 2
مجىء جبريل ليعلم المسلمين أمر دينهم
Kuja Kwa Jibriyl ('Alayhis-Salaam) Kuwafundisha Waislamu Mambo Ya Dini Yao
عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قَالَ: بَيْنَما نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَومٍ، إذْ طَلَعَ عَلَينا رَجُلٌ شَديدُ بَياضِ الثِّيابِ، شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عَلَيهِ أثَرُ السَّفَرِ، وَلا يَعْرِفُهُ مِنَّا أحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيهِ إِلَى رُكْبتَيهِ، وَوَضعَ كَفَّيهِ عَلَى فَخِذَيهِ.
وَقالَ: يَا مُحَمَّدُ، أخْبرني عَنِ الإسلامِ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((الإسلامُ: أنْ تَشْهدَ أنْ لاَّ إلهَ إلاَّ الله وَأنَّ مُحمَّدًا رسولُ الله، وتُقيمَ الصَّلاةَ، وَتُؤتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ البَيتَ إن اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبيلًا)). قَالَ: صَدَقْتَ. فَعَجِبْنَا لَهُ يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقهُ!
قَالَ: فَأَخْبرنِي عَنِ الإِيمَانِ. قَالَ: ((أنْ تُؤمِنَ باللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبهِ، وَرُسُلِهِ، وَاليَوْمِ الآخِر، وتُؤْمِنَ بالقَدَرِ خَيرِهِ وَشَرِّهِ)). قَالَ: صَدقت. قَالَ: فأَخْبرني عَنِ الإحْسَانِ. قَالَ: ((أنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاكَ)).
قَالَ: فَأَخْبِرني عَنِ السَّاعَةِ. قَالَ: ((مَا المَسْؤُولُ عَنْهَا بأعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ)). قَالَ: فأخبِرني عَنْ أمَاراتِهَا. قَالَ: ((أنْ تَلِدَ الأَمَةُ رَبَّتَهَا، وأنْ تَرَى الحُفَاةَ العُرَاةَ العَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ في البُنْيَانِ)).
ثُمَّ انْطَلقَ فَلَبِثْتُ مَلِيًّا، ثُمَّ قَالَ: ((يَا عُمَرُ، أَتَدْري مَنِ السَّائِلُ؟)) قُلْتُ: اللهُ ورسُولُهُ أعْلَمُ. قَالَ: ((فإنَّهُ جِبْريلُ أَتَاكُمْ يعْلِّمُكُمْ دِينَكُمْ)). رواه مسلم
‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa mbele ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa ghafla akatutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Rasuli) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Uislamu ni kukiri kuwa hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na Muhammad ni Rasuli wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga Swawm Ramadhwaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.” (Akasema yule mtu yaani Jibriyl): “Umesema kweli.” Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake Rasuli na kumsadikisha. Na akasema tena: Niambie kuhusu Iymaan. Akasema: “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rusuli Wake na siku ya Qiyaamah, na kuamini Qadar (majaaliwa ya Allaah) ya khayr zake na shari zake.” (Akasema Jibriyl): “Umesema kweli.”. Akasema: “Hebu nielezee kuhusu Ihsaan.” Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni kumuabudu Allaah kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.” Akasema (Jibriyl): “Niambie kuhusu Qiyaamah.” Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji.” Kisha akamwambia: “Nijulishe alama zake.” Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya fahari.” Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari). Kisha akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Allaah na Rasuli wake wanajua zaidi. Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.”
Comments
Post a Comment