SURA YA KWANZA VIPI TUTAMFAHAMU MOLA WETU NA WAPI TUICHUKUE IMANI YA DINI YETU? Hili ni swali muhimu mno na jawabu sahihi la swali hili ndiyo ufumbuzi wa matatizo mengi yaliyojitokeza katika umma wa kiislamu, kwa sababu waislamu wengi hawajui vipi watamfahamu mola wao muumba, na wapi wanatakiwa kuichukua dini yao ! Ama Ahlu Sunna wal Jama’a wao wanaitakidi kwamba: Tutamjua mola wetu kwa vile alivyojielezea yeye mwenyewe katika kitabu chake (Qur’an tukufu) na vile alivyotuelezea mjumbe wake mtukufu katika mafundisho yake yaliyo sahihi. Kwa kuyathibitisha yale yote ambayo Allah amejithibitishia mwenyewe au ambayo ameyathibitisha Mtume wake -swalla llaahu alayhi wasallam-, na kuzikanusha sifa ambazo Allah na Mtume wake swalla llaahu alaihi wasallam wamezikanusha, bila ya kupotosha, wala kupinga, wala kumfananisha yeye na chochote katika viumbe vyake, pamoja na kufuta dhana ya kwamba kuyathibitisha yale ambayo Allah amejisifia nayo kuwa ni kumfananisha y...
Posts
Showing posts from February, 2017