1. ADDIYNUN-NASIIHATU Dini ni nasaha Yaani ni nasaha kwa viumbe au kwa Mtume au kwa Mwenyezi Mungu. Ndiyo kusema kuwahurumia viumbe, kuishika dini ya Mwenyezi Mungu kwa uaminifu na kumsaidia Mtume katika kazi alizokabidhiwa na Mwenyezi Mungu. 2. IJTANIBUL GHADHWABA Jiepusheni na hasira Mara nyingi hasira inaleta matusi, magomvi na hata kuuana. 3. ADDUU ZAKAATAKUM Toeni zaka zenu Maana zaka ni msaada kwa mafukara na maskini na pia inatakasa mali ya mtu anayeitoa. 4. IHFADH LISAANAKA Linda ulimi wako Yaani usiwe na masingizio, uongo, utesi na maneno ya magomvi, machafuko, na maneno ya upuuzi. 5. ARHAAMUKUM ARHAAMUKUM Ndugu zenu ndio ndugn zenu Kwa hiyo wahurumieni, watendeeni mema, na wasaidieni zaidi kuliko wengine maana mmechangia damu. 6. ARSHIDUU AKHAAKUM Waongozeni ndugu zenu Kwa kuwafundisha na kuwapa mawaidha na kuwakataza maovu ili wawe watu wema. Üû ×øŠû iø Üû ×ô ‰û ]ø 7. ASLIM TASLAM Silimu utasalimika Mwenye kuishika dini ya Kiis...
Comments
Post a Comment