Posts

Showing posts from January, 2017

AYYOUBIYYAH DAY IMEANZA RASMI LEO HII.

Image
Leo ni cku ya kuanza kwa shughuli za madrasat Ayyoubiyyat mzingani ambazo zimefunguliwa rasmi asubuhi ya leo kwa visomo na dua mbalimbali. Zilizoongozwa na shekh Kogoda(shekh Muhammad khatwibu)  pamoja na NAibu wake shekh Ramadhwaani Mabrook. Shughuli hizo zinatarajiwa kuendelea jioni ya leo baada ya swala ya alasiri na khayimae kufikia hapo kesho saa 5 ucuku ambapo zitafungwa rasmi mpaka mwakani inshaalla. WAISLAMU WOTE MNAOMBWA KUHUDHURIA MKIWA NI WAPENZI WA MTUME. picha z a matukio mbali mbali katika ufunguzi huo. KARIBUNI SANA KARIBUNI PALIPO PENU.

NUKUU YA LEO

( قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ) الكهف (110) Al-Kahf Sema: Mimi ni mwanaadamu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.

NASAHA YA LEO

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada: Kutawasali Kwa Kutaja Hali Na Kutaja Sababu Nasiha Mbali Mbali Inafaa kutawassal kwa kutaja hali au sababu ya jambo unaloliombea du'aa. Ikiwa jambo unaloliomba ni kwa ajili ya manufaa ya dunia, basi  liwe ni jambo lenye kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na linalokubalika katika shariy’ah.  Mifano mingi imo katika Qur-aan waliyoomba Manabii. Mifano michache ifuatayo: Nabiy Nuwh ('Alayhis-Salaam):   Aliomba nusra baada ya kushindwa kuwalingaia watu wake miaka mia tisa na khamsini. [Al-‘Ankabuwt 29: 14]. Katika Suwratul-Qamar Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:    كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُونٌ وَازْدُجِرَ ﴿٩﴾ Walikadhibisha kabla yao kaumu ya Nuwh, wakamkadhibisha mja Wetu, wakasema: “Majnuni.” Na akakaripiwa. Nabiy Nuwh ('Alayhis-Salaam) akaomba: فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانتَصِرْ ﴿١٠﴾ Basi a...

HADITHI 40

    1. ADDIYNUN-NASIIHATU Dini ni nasaha Yaani ni nasaha kwa viumbe au kwa Mtume au kwa Mwenyezi Mungu. Ndiyo kusema kuwahurumia viumbe, kuishika dini ya Mwenyezi Mungu kwa uaminifu na kumsaidia Mtume katika kazi alizokabidhiwa na Mwenyezi Mungu. 2. IJTANIBUL GHADHWABA Jiepusheni na hasira Mara nyingi hasira inaleta matusi, magomvi na hata kuuana. 3. ADDUU ZAKAATAKUM Toeni zaka zenu Maana zaka ni msaada kwa mafukara na maskini na pia inatakasa mali ya mtu anayeitoa. 4. IHFADH LISAANAKA Linda ulimi wako Yaani usiwe na masingizio, uongo, utesi na maneno ya magomvi, machafuko, na maneno ya upuuzi. 5. ARHAAMUKUM ARHAAMUKUM Ndugu zenu ndio ndugn zenu Kwa hiyo wahurumieni, watendeeni mema, na wasaidieni zaidi kuliko wengine maana mmechangia damu. 6. ARSHIDUU AKHAAKUM Waongozeni ndugu zenu Kwa kuwafundisha na kuwapa mawaidha na kuwakataza maovu ili wawe watu wema. Üû ×øŠû iø Üû ×ô ‰û ]ø 7. ASLIM TASLAM Silimu utasalimika Mwenye kuishika dini ya Kiis...

MATUKIO MBALIMBALI

Image
ASSALAAMU ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKAATUH VIJANA wa almadrasatul Shamsiyyat wakiwa katika shughuli za kusherehekea mazazi ya Mtume MUHAMMAD (s.a.w) katika kijiji cha Mwambani wilaya ya Tanga Mjini. Hafla hiyo ilidhuriwa  na viongozi mbalimbali wa DINI akiwemo sheikh, MUHAMMAD KHATWIBU (KIGODA) ambae ni mudiri wa madrasa hiyo, sheikh Ramadhani Mabrouk(naibu mudiri), sheikh Husein Hashimu na walimu mbalimbali kutoka sehemu tofauti. SHEIKH KIGODA AKIWA KATIKA HADHARA HIYO MWALIMU WA MADRASA HIYO NA WANAFUZI WAKIWA KATIKA ZAFA KWAKWELI HADHARA ILIPAMBIKA VILIVYO USTAADH ALLY TAJIRI (MWAKIDOSHO) AKIWA MAKINI KATIKA  SHUGHULI HIYO PAMOJA NA USTAADH OMARI HAMZA

KARIBU AYYOUBIYYAT

Image
AYYOUBIYYAT MZINGANIL AALAA